Wiki
chache zilizopita mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid Cristiano
Ronaldo alitangaza ujio wa mavazi yake mapya kupitia label yenye
ufupisho wa jina lake ‘CR7′ lakini biashara yake hiyo inaweza kupata
tatizo nchini Marekani.
Kuna uwezekano mkubwa Ronaldo akashindwa
kuuza mavazi yake yenye lebo ya ‘CR7′ Marekani baada ya mtu mmoja nchini
humo kufungua kesi dhidi ya mshambuliaji huyo wa Real Madrid kutokana
na matumizi ya nembo ya “CR7″.
Christopher Renzi ambaye alilisajili jina la
“CR7″ kibiashara (akiunganisha herufi za kwanza za majina yake na tarehe
yake ya kuzaliwa: 7th October) nchini Marekani 2009 kwa matumizi ya
website yake pamoja na label yake ndogo ya mavazi, aliandikiwa barua
mara kadhaa na kampuni ya JBS Textile Group inayotengeneza bidhaa za
‘CR7′ za Cristiano Ronaldo, wakimwambia aache kutumia nembo hiyo.
JBS
pia wameiandikia barua ofisi ya usajili wa nembo za kibiashara ya
Marekani ili waweze kuwapatia haki ya kutumia jina nembo hiyo nchini
humo lakini pamoja na hilo, Renzi nae amefungua kesi dhidi ya JBS na
Ronaldo ili aweze kutajwa kisheria kabisa kuwa mmiliki halali wa leseni
ya nembo ya ‘CR7′ kwenye mipaka ya Marekani.
Kwenye maongezi na shirika la habari la Marekani Reuters, mwanasheria wa Renzi alisema “Tunachohitaji na wao kutuacha huru bila usumbufu.”